IQNA

Taifa la Iran laadhimisha mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

15:35 - February 10, 2021
Habari ID: 3473638
TEHRAN (IQNA) - Sambamba na kutimia mwaka 42 tangu Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi nchini Iran chini ya uongozi wa hayati Imam Ruhullah Khomeini, wananchi wa Iran tangu mapema leo asubuhi wameghariki katika sherehe za kuenzi na kuadhimisha tukio hilo ambazo mwaka huu zinafanyika kwa sura tofauti kutokana na sheria kali za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

Wananchi wa Iran katika maeneo mbalimbali ya nchi wanashiriki katika sherehe za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa harakati ya magari na pikipiki kote nchini ili kulinda sheria za kukabiliana na mambukizi ya corona.

Kutokana na sheria hizo, mikusanyiko ya watu imepigwa marufuku katika sherehe za leo za Mapinduzi ya Kiislamu na sherehe hizo zinafanyika kwa misafara na harakati za magari na mapikipiki ya wananchi katika mitaa ya miji na vijiji vya Iran.

Sambamba na sherehe hizo zinazoendelea katika maeneo mbalimbali ya Iran, Rais Hassan Rouhani alikuwa akihutubia taifa na kueleza mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoyakabili Mapinduzi ya Kiislamu tangu miaka 42 iliyopita.

Leo tarehe 22 Bahman kwa mwaka wa Hijria Shamsia inaadhimishwa hapa nchini kwa mnasaba wa kutimia miaka 42 tangu Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi kamili na kuuondoa madarakani utawala wa kifalme na kibaraka nchini Iran. Mapinduzi hayo yaliongozwa na Imam Ruhullah Khomeini , Mwenyezi Mungu Amrehemu, ambaye ni muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

3953308

captcha