IQNA

Matayarisho ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza

10:10 - October 30, 2021
Habari ID: 3474490
TEHRAN (IQNA)- Matayarisho ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani yameanza huku nchi kadhaa zikiwa tayaris zimeshatangaza kuwa tayari kushiriki.

Mehdi Ghare-Sheikhlou, mkuu wa masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu la Iran amesema hadi sasa nchi 53 zimeshawasilisha majina ya wawakilishi wao katika mashindano hayo.

Akizungumza katika mahojiano na Televisehni ya Qur'ani ya Iran Ijumaa, afisa huyo amesema mashindano hayo ya kimataifa yatakuwa na vitengo vine vya wanaume, wanawake, wanafunzi wa shule na wenye ulemavu wa macho.

Halikadhalika amebaini kuwa duru ya mchujo ya mashindano hayo itafanyika kwa njia ya intaneti ambapo watakafaul watashiriki fainali katika mashindano yatakayofanyika nchini Iran.

Aidha aimesema nchini Iran fainali ya mashindano ya 44 ya kitaifa ya Qur'ani itafanyika  mwezi Novemba/Disemba.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashhindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ambao washindani kutoka kila kona ya dunia hushiriki.

Duru ya 37 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ilifanyika Machi 6-11 mwaka huu kwa kuzishirikisha nchi 67.

4008795

captcha