IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Zaidi ya Nchi 90 kuhudhuria Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran

21:33 - October 28, 2023
Habari ID: 3477801
TEHRAN (IQNA) - Idadi ya nchi zinazotarajiwa kushiriki katika toleo lijalo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ni zaidi ya 90, imedokezwa.

Hamid Majidimehr, ambaye anaongoza kituo cha masuala ya Qur'ani cha Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada Iran, aliyasema hayo katika kikao cha kamati hiyo kwa ajii ya kuendeleza shughuli za uenezaji na ukuzaji wa Qur'ani Tukufu.

Mkutano huo ulifanyika mapema wiki hii na kuongozwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili.

Katika hotuba yake kwenye kikao hicho, Majidimehr alisema kuna mashindano mawili tu ya kimataifa ya Qur'ani duniani ambapo zaidi ya nchi 80 zinashiriki na Iran ni mojawapo.

Alisema kutokana na ushirikiano kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, Wizara ya Mambo ya Nje, na vyombo vingine idadi ya washiriki inatarajiwa kwa kubwa mwaka huu.

Finali ya Duru ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran imepangwa kuandaliwa mapema mwaka 2024.

Hafla hiyo huandaliwa kila mwaka na Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada la Iran kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

Duru ya mwisho ya toleo la 39 ilifanyika mnamo Februari 18, 2023, Tehran.

Kauli mbiu ya toleo hili, kama lile lililotangulia, ilikuwa "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria umuhimu ambao Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaipa kadhia ya umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

 

4177601

Habari zinazohusiana
captcha