IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Ratiba ya fainali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yatangazwa

19:01 - February 09, 2023
Habari ID: 3476538
TEHRAN (IQNA) - Waandaaji wametangaza ratiba ya fainali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ambayo yanatarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, sherehe za uzinduzi zitafanyika Februari 18, sambamba na Siku ya Maba'ath (kuteuliwa kwa Mtume Muhammad-SAW-kama mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu) kuanzia saa kumi alasiri hadi 12 jioni kwa wakati wa Tehran.

Mashindano ya kategoria za wanaume yatafanyika Februari 19-21 kutoka kuanzia saa tisa alasiri hadi saa tatu usikui.

Mashindano ya kategoria za wanawake pia yatafanyika mnamo Februari 19-20 kutoka saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

Kategoria hizo ni pamoja kuhifadhi, na kusoma Qur'ani Tukufu kwa wanaume na  wanawake.

Sherehe ya kufunga imepangwa kufanyika Februari 22 saa kumi jioni.

Mchakato wa tathmini katika duru ya awali ya shindano hilo ulihitimishwa katikati ya Januari.

Jumla ya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Tukufu 149 kutoka nchi 80 wakiwemo wanaume 114 na wanawake 35 walishiriki katika duru ya kwanza.

Kauli mbiu ya mashindano yam waka huu ni kama ya mwaka uliopita nayo  ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", na ni ushahid kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa uzito mkubwa suala na umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfuna Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

3482118

captcha