IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran: Wajumbe wa Majopo ya Majaji watangazwa

20:41 - January 10, 2023
Habari ID: 3476380
TEHRAN (IQNA) - Kamati ya maandalizi ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran imetangaza majina ya wataalamu wa Qur'ani watakaohudumu katika majopo ya majaji wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfu na Misaada, Mohammad Javad Rajaei, Nosratollah Hosseini, Saeed Fayaz, Reza Mohammadpour na Mohammad Sadeq Nasrollahi watakuwa wajumbe wa jopo katika sehemu ya wanaume.

Wataalamu wawili wa kigeni wa Qur'ani, Ahmed Adel Abdilbari kutoka Iraq na Seyed Ahmad Ghaffari kutoka Afghanistan pia watahudumu katika jopo hilo.

Jopo hilo la wanaume litaongozwa na Seyed Ali Sarabi huku Hashem Roghani akiwa msimamizi wa ufundi.

Kwa upande wa wanawake, Maryam Khatib atakuwa mwenyekiti wa jopo la majaji na Azam Almasi atakuwa msimamizi wa ufundi.

Kuanzia Januari 23 hadi 27, watatathmini faili zilizorekodiwa za wagombea wanaoshiriki katika hatua ya awali ya machukjo.

Jumla ya wasomaji Qur'ani Tukufu 146 kutoka nchi 80 wametuma faili zao za qiraa katika sekretarieti ya mashindano hayo.

Fainali hizo ambazo zimepangwa kufanyika kwa njia ya kuhudhuria washiriki katika ukumbi zitaanza Februari 13, sambamba na Siku ya Maba’ath (kuashiria kuteuliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) kuwa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu).

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

  4113537

captcha