IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran yaonyesha vipawa

19:43 - January 14, 2023
Habari ID: 3476402
TEHRAN (IQNA) - Washindani wanaendelea kuonyesha vipaji vyao katika duru ya mwisho ya toleo la 45 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika kipindi Ijumaa asubuhi kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima. Saeed Aliakbari kutoka Mkoa wa Qazvin alikuwa wa kwanza kujibu maswali ya jopo la waamuzi.

Washiriki wengine ambao zamu yao ilikuja siku ya kwanza walikuwa kutoka majimbo ya Golestan, Mazandaran na Gilan.

Katika kikao cha alasiri, washindani wa kategoria ya usomaji au qiraa walianza kuwania tuzo ya juu, na wale kutoka majimbo ya Tehran na Razavi Khorasan wakiwa miongoni mwa waliofanya vizuri.

Tarteel na kuhifadhi Juzuu 20 za Qur’ani Tukufu  ni kategoria zingine katika mashindano.

Mashindano hayo ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu Iran yalianza rasmi katika sherehe huko Ahvaz, mji mkuu wa jimbo la Khuzetsan kusini-magharibi siku ya Alhamisi na yanatazamiwa kumalizika  Jumatano Januari 17.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya shindano hilo ambapo majaji watatumia mfumo wa kidijitali kutathmini uwezo wa washiriki.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na huandaliwa Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada kwa kushirikisha wanafunzi na wanaharakati bora wa Qur’ani Tukufu kutoka kote nchini.

Mashindano hayo yanalenga kugundua vipaji vya Qur'ani na kukuza shughuli za Qur'ani sambamba na kuhimiza utekelezwaji wa mafundisho ya Qur’ani nchini.

4114402

captcha