IQNA

Jinai za Israel

Hamas: Palestina si mahala pa utawala ghasibu wa Israel

18:56 - December 15, 2022
Habari ID: 3476254
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, anasema ardhi ya Palestina si mahala pa utawala vamizi na ghasibu wa Israel.

Katika hotuba ya kuadhimisha miaka 35 tokea ilipoanzishwaHamas, Ismail Haniyeh amesisitiza kwamba Hamas "imejitolea inafungamana na misimamo yake ya kisiasa."

Hamas "ina mkakati wa wazi na usioyumba kuhusu kadhia ya ukombozi wa Palestina na mapambano dhidi ya Wazayuni wakoloni," alielezea.

Harakati hiyo "ilipitisha mkakati wa uwazi kwa mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu na imeanzisha uhusiano wenye usawa kwa msingi kwamba kadhia ya Palestina ni muhimu kwa ulimwengu wote wa Kiarabu na Kiislamu."

"Hamas kwa muda mrefu imekuwa ikijitolea kwa umoja wa watu wa Palestina ndani na nje ya nchi ili kukabiliana na  uvamizi wa Israel na mipango yake," Haniyeh alisema.

Alikariri kuwa Wapalestina "kamwe hawataruhusu uvamizi wa Israel kutekeleza mipango yake ovu inayolenga Al Quds (Jerusalem), kwa ujumla, na Msikiti wa Al-Aqsa, haswa."

Akitoa salamu kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoteseka katika magereza yanayokaliwa na Israel, Haniyeh alikariri kuwa Hamas haitabakisha juhudi zozote za kuwaachilia huru.

4107227

captcha