Katika taarifa yake, baraza hilo lilisema kuwa linafuatilia "ukiukaji hatari unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Al Quds," likibainisha kuwa "mashuhuri zaidi ni uvamizi wa wanasiasa wa Israel ambao wanafuata itikadi kali kuhusiana na Msikiti wa Al-Aqsa."
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanasiasa wa Israel wanaouvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa hutumia sikukuu za Kiyahudi kama kisingizio cha kufichua sera zao za Uyahudishaji maeneo hayo matakatifu..
"Makundi ya Wayahudi yenye msimamo mkali yalitekeleza ibada za kizushi na za uchochezi, ikiwa ni pamoja na kuimba ndani ya yadi takatifu za Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa," ilisema taarifa hiyo.
Hii ilikuja kufuatia uvamizi wa mamia ya Waisraeli wa mrengo wa kulia wakati wa likizo ya Kiyahudi ya Hanukkah.
Baraza hilo limekuwa likifuatilia "kwa wasiwasi mkubwa" mienendo ya mamlaka ya uvamizi ya Israel na "kampeni za kimfumo za uchochezi" ambazo zinalenga Waislamu kote ulimwenguni.
Baraza la Wakfu la Jordan limetaka Israel kuacha tabia za "kibaguzi na uchochezi" na kuacha kuwatumia walowezi wenye itikadi kali kutekeleza mipango yao ya Uyahudi kabla ya vita vya kidini kuzuka.
3481861