IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina 13,000 wanakaribia kuhamishwa kwa nguvu kutoka Al-Quds

19:33 - January 13, 2023
Habari ID: 3476398
TEHRAN (IQNA) - Afisa mmoja wa Palestina anasema takriban wakazi 13,000 Wapalestina katika mji wa al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu huenda wakalazimika kuyahama makazi yao kutokana na sera za utawala ghasibu wa Israel.

Raia wa al-Quds wapatao 13,000 wanatishiwa kuhama kwa lazima kutoka ardhi zao za jadi katika Jiji la Kale la al-Quds linalokaliwa kwa mabavu ili kupisha nyumba za Wayahudi pekee, masinagogi, bustani na makumbusho ya Biblia, Mshauri wa Ofisi ya Rais wa Palestina kuhusu Masuala ya al Quds, Ahmed Al-Ruwaidi, alionya. .

Katika taarifa yake, Al-Ruwaidi alisema uchimbaji unatokelekezwa na  mamlaka ya Israel na ufunguzi wa mahandaki katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa unalenga kuimarisha makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo la Mji Mkongwe wa al  Quds, na kuwalazimisha Wapalestina eneo hilo waondoke kwa kuhofia uchimbaji uliofanywa chini ya nyumba zao au sera ya uhamishaji wa kulazimishwa inayotekelezwa na mamlaka ya Israeli dhidi yao kwa miaka kadhaa.

Alidokeza kwamba utawala wa kikoloni  wa Israel unataka kuwasilisha masimulizi bandia ya Talmudi ambayo hayana msingi wa kihistoria kwa gharama ya ukweli wa kihistoria wa turathi za Waarabu wenye asili Kanaani.

"Tumekuwa tukifanya kazi kwa miezi kadhaa kukusanya hati kubwa zaidi za kihistoria zinazoakisi ukweli kuhus Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na maeneo  yake ya karibu," alisema na kusisitiza kwamba hati na simulizi zote za zamani na za Uthmaniyya hadi leo zinathibitisha kwamba mji wa  al-Quds ni wa Kiarabu wenye historia ya  Kiislamu na Kikristo.

"Nyaraka zote zilizokusanywa zina ukweli sawa wa kihistoria, na hazitoi dalili yoyote ya simulizi yoyote ya Talmudi ambayo utawala vamizi wa Israel unajaribu kukuza," Al-Ruwaidi alisema, akitoa wito kwa UNESCO kubeba majukumu yake ya kisheria kwa kutuma dharura. kamati ya uchunguzi kuchunguza ukiukaji wa urithi wa kitamaduni huko Jerusalem, ambao umesajiliwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia tangu 1981.

Utawala wa Kizayuni unachukua hatua hizo za kibeberu kuhusiana na mji wa al-Quds na msikiti wa Al Aqsa wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO lilipitisha azimio mwaka 2016 lililopinga kuwepo uhusiano wowote wa kihistoria, kidini au kiutamaduni kati ya Mayahudi na maeneo matakatifu ya mji wa al-Quds na hasa msikiti wa Al Aqsa na kusisitiza kuwa, msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

3482054

captcha