IQNA

Quds Tukufu

Wiki ya Kimataifa ya Al-Quds yazinduliwa kwenye mitandao ya kijamii

17:46 - February 15, 2023
Habari ID: 3476566
TEHRAN (IQNA) – Mpango wa Wiki ya Kimataifa ya Al-Quds umezinduliwa na mwanaharakati kwenye mitandao ya kijamii kuangazia changamoto zinazoukabili mji huo mtakatifu ambao pia unajulikana kama Jerusalem.

Makundi na mashirika ya Kiislamu, yakiwemo Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) na Umoja wa Wanazuoni wa Palestina, yote yalishiriki katika hafla hiyo.

Sheikh Dr Ali Mohiuddin al-Qaradaghi, katibu mkuu wa IUMS, alitoa wito kwa kila mtu kushiriki katika mpango huo kwa kuzungumzia suala hilo kwenye mitandao ya kijamii, kufanya mikutano na kufanya mahojiano na vyombo vya habari.

"Waislamu wote duniani ni washirika katika Palestina," alisema Mwanazuoni wa Kiislamu wa Mauritania Sheikh Mohammad Al Hassan Ould Al Dadou. "Huu ni wakati mzuri wa kufanya kazi kwa Palestina, al-Quds na Msikiti wa Al-Aqsa." Mji wa Al Quds unakaliwa kwa mabavu na kukol;oniwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao pia unakoloni ardhi zingine za Palestina. 

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel, ambapo unakalia Palestina kwa mabavu, umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina katika mji wa Al Quds na maeneo mengine ya Palestina ambayo unayakalia kwa mabavu.. Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu uko katika mji wa Al Quds na umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Kando ya Wiki ya Al-Quds Ulimwenguni, Jukwaa la Al Quds Amanati la Wasudan lilieandaa kikao kuhusu hatua ya kisaliti ya Sudan kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel na kulaani uamuzi huo sambamba na kusema ni hatari ya kistratijia kwa Khartoum.

3482496

captcha