IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Mashindano ya Qur'ani ya Al-Azhar: Takriban washiriki 60,000 waingia katika hatua ya pili

19:21 - January 20, 2023
Habari ID: 3476437
TEHRAN (IQNA) – Matokeo ya hatua ya awali ya mashindano ya nchi nzima ya Qur'ani Tukufu Misri yanayoendeshwa na Al-Azhar Islamic Center yametangazwa.

Kulingana na tangazo hilo, washiriki 59,495 wamefika katika hatua inayofuata ya hafla hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Februari 25.

Mashindano hayo ya Quran Tukufu ambayo yanasimamiwa Sheikhe Mkuu wa Kituo chya Kiislamu cha Al Azhar yalikuwa na washiriki 180,000 katiukak hatua ya awali ambayo ilifanyika hivi karibuni.

Wale watakaopata angalau pointi 80 kati ya 100 watafuzu kwa raundi inayofuata, yaani hatua ya kikanda.

Wagombea wakuu watashindana katika duru ya mwisho, iliyopangwa kufanyika katika mji mkuu Cairo.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Idara ya Masuala ya Qur'ani ya Al-Azhar kwa ajili ya wanafunzi wa Al-Azhar na vituo vyake vya kuhifadhi Qur'ani.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani ni maarufu katika nchi hiyo ambayo ina baadhi ya wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu duniani.

 

4115935

captcha