IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Maadui wanatumia mbinu mpya ya kuanzisha vita, uvamizi na hujuma ya kiutamaduni dhidi ya Iran

21:40 - February 24, 2023
Habari ID: 3476616
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema aada ya miaka minane ya vita kamili vya kijeshi na kiuchumi vilivyomalizika kwa ushindi wa Iran ya Kiislamu, maadui wanatumia mbinu mpya ya kuanzisha vita, uvamizi na hujuma ya kiutamaduni dhidi ya Iran.

Hujjatul-Islam Kazem Sediqi, hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa tangu siku ya kwanza ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, madola makubwa ya Mashariki na Magharibi yalifanya mikakati ya kutoa dharuba dhidi ya Mapinduzi hayo na kuongeza kuwa: Maadui wa Iran ya Kiislamu wanatumia mbinu za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita laini na kuchochezi kaumu tofauti kwa lengo la kuzusha hitilafu za ndani, lakini unjama hizo zimefeli na kushindwa kutokana na tadbiri ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na mshikamano na uungaji mkono na wananchi.

Kwingineko Khatibu wa Sala ya Ijumaa amekosoa hatua ya serikali ya Ujerumani ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Iran na kusisitiza ulazima wa kukabiliana ipasavyo na kitendo hicho.

Ujerumani umechukua hatua hiyo baada ya Idara ya Uhusiano wa Umma ya Mahakama ya Mkoa wa Tehran kutangaza Jumanne iliyopita kwamba, baada ya kukamilika upelelezi na uchunguzi, Mahakama ya Mapinduzi ya Tehran imempata na hatia na kumhukumu kifo Jamshid Sharmahd, kiongozi wa kundi la kigaidi la Tondar kwa tuhuma za kufanya uharibifu katika nchi kupitia njia ya kupanga na kuelekeza vitendo vya kigaidi.

Baada ya kutangazwa hukumu ya kifo dhidi ya kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la Tondarr, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani iliimwita balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Berlin na kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Iran.

 

Hujjatul-Islam Kazem Sediqi, hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, amedokeza kuwa Jamshid Sharmahd, kiongozi wa kundi la kigaidi la Tondar, amehukumiwa kifo mbele ya wakili na katika mahakama ya haki, na amekosoa mienendo ya serikali ya Ujerumani ya kuingilia kati suala hili.

Amesema: Serikali ya Ujerumani na vyombo vya habari vinavyopinga ubinadamu vimelivalia njunga suala hili, kiasi kwamba Berlin imewafukuza baadhi ya wanadiplomasia wa Iran; hivyo kuna ulazima Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ikabiliane ipasavyo na hatua hiyo ya kijeuri.

Jamshid Sharmahd alikabiliwa na tuhuma za kupanga mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi dhidii ya taasisi za kidini na kiuchumi nchini Iran, ikiwa ni pamoja na shambulio la bomu la mwaka 2008 katika kituo cha kidini cha Sayyid al Shuhadaa huko Shiraz, ambapo watu 14 waliuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.

4124090

captcha