IQNA

Jinai za Israel

Vikosi vya Israel vyazuia adhana katika Msikiti wa Al-Aqsa

16:50 - April 25, 2023
Habari ID: 3476912
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya utawala ghasibu wa Israel siku ya Jumatatu vilimzuia mwadhini katika Msikiti wa Al-Aqsa katika jiji la Al-Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu kukamilisha.

Hatua hiyo ilikuwa kwa kisingizio cha sherehe za walowezi wa Kizayuni katika ua wa Ukuta wa Magharibi (Medani ya Al-Buraq) wa jengo la Msikiti wa Al-Aqsa, kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Palestina Wafa.

Mapema Jumatatu pia, walowezi kadhaa wa Kiyahudi-Kizayuni waliokuwa wakisindikizwa na polisi katili wa Israel walivamia msikiti huo mtakatifu, alisema Wafa.

Mvutano kati ya Israel na serikali ya Jordan, ambayo ni msimamozi rasmi wa Msikiti wa Al-Aqsa, umekuwa mkubwa katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa Israel katika eneo la msikiti huo.

3483330

captcha