IQNA

Quds Tukufu

Mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa asailiwa na maafisa wa Kizayuni

11:15 - December 18, 2023
Habari ID: 3478052
IQNA - Sheikh Ekrima Sabri, mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem), aliitwa na mamlaka ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhojiwa siku ya Jumapili.

"Sheikh Sabri alihojiwa kuhusu tuhuma za uchochezi katika Kituo cha Mahabusu cha Moscovia huko Jerusalem," Hamza Qutina, wakili wake wa utetezi, alisema katika taarifa zilizotajwa na shirika la habari la Wafa.

Maafisa wa kijasusi wa Israel walivamia nyumba ya Sheikh Sabri mnamo Desemba 4 na kumpiga marufuku ya kusafiri.

Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 84 alizuiliwa mara kadhaa na Israel na alipigwa marufuku kuingia Msikiti wa Al-Aqsa kwa miezi kadhaa.

Sabri ni mkosoaji mkubwa wa uvamizi wa Israel wa miongo kadhaa katika maeneo ya Wapalestina. Hapo awali aliwahi kushika wadhifa wa mufti wa Al Quds na maeneo ya Palestina kuanzia 1994 hadi 2006.

Msikiti wa Al-Aqsa ni eneo la tatu kwa utakatifu duniani kwa Waislamu. Wayahudi huliita eneo hilo "Mlima wa Hekalu," wakidai kuwa palikuwa na mahekalu mawili ya Kiyahudi katika nyakati za kale.

Israel iliikalia kwa mabavu Mashariki ya al-Quds, ambako umo Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa Vita vya Waarabu na Israel vya mwaka 1967. Utawala ghasibu wa Isareli ulinyakua jiji hilo lote mwaka wa 1980, hatua ambayo haikutambuliwa kamwe na jamii ya kimataifa.

3486456

Habari zinazohusiana
captcha