IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Waliowashambulia Waislamu Toronto, Kanada wakamatwa

16:26 - May 19, 2023
Habari ID: 3477015
TEHRAN (IQNA) – Mashambulizi mengi dhidi ya Waislamu yameripotiwa karibu na Toronto nchini Kanada (Canada) huku polisi wakikamata watu baada ya uchunguzi.

Polisi wa Kanada walimkamata mwanamume aliyejaribu kuwagonga waumini wa Kiislamu kwenye misikiti miwili katika eneo la Greater Toronto Area, na huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu "wenye chuki dhidi Uislamu."

Polisi walisema waliitwa wakati wa ibada katika msikiti wa Toronto baada ya mwanamume mmoja kudaiwa kuliendesha gari lake hadi kwenye eneo la kuegesha magari na kujaribu kuwagonga waumini pamoja na magari mengine.

Kisha dereva akaondoka kwa kasi na kwenda kwenye msikiti mwingine na kurudia vitendo vile vile. Matukio hayo yalitokea Aprili 5 baina ya saa 11 unusu hadi 12 asubuhi, polisi walisema.

Kisha mshukiwa huyo aliendesha gari hadi kwenye jumba la maduka la Scarborough, ambako aliingia na kuwakabili wanunuzi kadhaa kwa njia ya vitisho na kupiga kelele dhidi ya Waislamu.

Kijana mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa mawili ya uendeshaji hatari wa gari, makosa matano ya unyanyasaji wa jinai, kutoa vitisho vya kudhuru mwili, kushambulia na kufanya vitendo vichafu hadharani na kuwatusi wengine.

Polisi pia waliishia kumshtaki mshukiwa kwa tukio lingine mnamo Aprili 7 katika msikiti mmoja katika jiji la karibu la Markham.

Katika tukio tofauti katika mji wa Kitchener takriban kilomita 100 (maili 62.1) magharibi mwa Toronto, polisi walimfungulia mashtaka mwanamke wa umri wa miaka 27 baada ya shambulio linalodaiwa kuwa la chuki lililotokea wakati watu wakisubiri kwenye kituo cha mtihani wa udereva siku ya Jumatano.

3483611

captcha