IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yavutia nchi 52

15:11 - August 20, 2023
Habari ID: 3477467
KUALA LUMPUR (IQNA) Mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yalianza rasmi Jumamosi usiku katika mji wa Kuala Lumpur.

Hafla hiyo, ambayo inajulikana rasmi kama Mkutano wa Kimataifa wa Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani ya Malaysia (MTHQA), ilianza katika Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Kuala Lumpur, huku wananchi washindani, na maafisa wa ngazi za juu wakihudhuria.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 wamepangwa kushindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani. Kwa mujibu wa taarufa, wanaume 24 na wanawake 12 wanashindana katika kitengo cha usomaji ambacho kinafanyika jioni, na wanaume 27 na wanawake 13 katika kitengo cha kuhifadhi  kinafanyika  asubuhi.

Matukio yote yanaonyeshwa moja kwa moja kutoka kwa akaunti za mitandao ya kijamii za Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM). Mashindano hayo yatakamilika Agosti 24.

Akihutubia sherehe za ufunguzi, Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim alisema kuwa mashindano hayo ni juhudi za kuongeza uelewa wa kitabu hicho kitakatifu.

Alisema Waislamu wanapaswa kusoma na kuithamini Qur'ani Tukufu ili kuweza kutoa maelezo na ufahamu kwa watu wa rangi na dini mbalimbali.

Kukuza uelewa kuhusu Qur'ani Tukufu kunaweza kukabiliana na Uislamu na kudhalilishwa

Afisa huyo wa Malaysia pia alisema kuwa chuki dhidi ya Uislamu iliyotokea duniani ilitokana na baadhi ya vyama ambavyo vilikuwa na mawazo ya juu juu kuhusu Uislamu.

"Ndio maana wakati tukio la kuchomwa kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi, mbali na kulaani, niliamua kuagiza kuchapishwa kwa Qur'ani Tukufu katika lugha zote zikiwemo za Kiswidi."

"Nakala  15,000 za Qur'ani Tukufu zimetumwa nchini Uswidi ili zisambazwe kwenye vyuo vikuu na vituo vya masomo ili waweze kutathmini na kusoma, na kwangu mimi, kwa serikali, hatua hii ni ya busara zaidi kuwapa ufahamu (wa Uislamu)," alisema.

3484842

Habari zinazohusiana
captcha