IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 21

Surah Al-Anbiya; Maelezo ya Qur'ani ya Wafuasi wa Kweli wa Dini

15:49 - October 19, 2022
Habari ID: 3475955
TEHRAN (IQNA) – Hadithi za Mitume 16 wa Mwenyezi Mungu zimetajwa katika Sura Al-Anbiya ya Qur’ani Tukufu ili kudhihirisha ukweli kwamba Mitume wote walifuata njia moja na walifuata lengo moja na kwamba wafuasi wao wote ni Ummah mmoja.

Surah Al-Anbiya ni sura ya 21 ya Qur'ani Tukufu. Ni Makki, ina Aya 112 na imo katika Juzuu ya 17 ya Kitbu Hicho Kitukufu. Ni Sura ya 73 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Katika aya ya 48 hadi 90 ya Sura hii kuna majina ya manabii 16 wa Mwenyezi Mungu. Aya pia zinazungumza juu ya Mtume Muhammad (SAW) na Mtume Isa (SAW) bila ya kuwataja. Kwa hiyo jina la Sura likawa ni Al-Anbiya (Mitume).

Sura hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) muda mfupi kabla ya kuondoka Makka kwenda Madina wakati ambapo watu wa Makka walikuwa katika hali ya kujikweza na kutomjali Mtukufu Mtume (SAW) na Qur'ani Tukufu. Ndiyo maana katika Sura hii imeelezwa hatima ya makafiri na Mushrikeen (washirikina), ambayo si chochote ila kukabiliwa na adhabu kali ya Mwenyezi Mungu.

Maudhui ya Sura kwa ujumla yanaweza kugawanywa katika sehemu mbili: imani na hadithi za kihistoria. Katika sura ya kwanza, Sura inaelekeza kwenye matokeo ya kupuuza Siku ya Kiyama, Wahy, na ujumbe wa Mitume. Aidha kutozingatia kwa watu maagizo na maonyo ya manabii kumetajwa

Baada ya kuwaonya wanaompinga Mtukufu Mtume Muhammad  (SAW), Sura inasimulia hadithi za Musa (AS) na Harun (AS), Ibrahim (AS), Lut (AS), Nuh (AS), Davoud (AS), Suleiman (AS). ), Ismail (AS), Idris (AS), Yunus (AS), Zakariya (AS), na Bibi Maryam (SA). Inamalizia kwa kusimulia hadithi hizi kwamba Mwenyezi Mungu amewafanya wafuasi wa imani zote kuwa Ummah Wahida (taifa moja), ingawa umoja huu wakati mwingine umedhoofika kwa sababu tofauti.

 Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi. Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu." (Aya ya 92-93 ya Surah Al-Anbiya)

Katika ulimwengu wa leo, wengine wanafikiri kwamba kauli mbiu ya Uislamu ya Umma Wahida inataka kukuza Uislamu na kuondoa imani nyingine. Hii ni katika hali ambayo wafuasi wa dini zote wanaweza kuishi pamoja kwa amani kwa kuzingatia mambo ya kawaida na kuheshimu imani ya kidini ya mtu mwingine. Kwamba umoja huo haujapatikana ni kwa sababu ya matakwa ya kupita kiasi na kutafuta madaraka ya makundi fulani. Kama kungekuwa na umoja wa namna hii miongoni mwa wafuasi wa dini mbali mbali, madhalimu na wakandamizaji hawangepata madaraka. Qur'ani Tukufu, hata hivyo, inatoa habari njema kwamba watu wema watairithi ardhi na utawala wa uadilifu na usawa utaenea duniani. “Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.” (Aya ya 105 ya Surah Al-Anbiya).

captcha