IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /48

Habari njema ya kudhihirisha ushindi kwa Waislamu katika Surah Al-Fath

10:55 - December 18, 2022
Habari ID: 3476265
TEHRAN (IQNA) – Moja ya matukio yenye maamuzi makubwa kwa Waislamu katika miaka ya mwanzo baada ya ujio wa Uislamu lilikuwa ni kutiwa saini kwa Mkataba wa Hudaybiyyah.

Mkataba huo ulipelekea kusitishwa kwa mapigano kwa miaka kumi kati ya Waislamu na makafiri. Tukio hilo yamkini likaonekana kuwa la kawaida lakini amani ilileta ushindi mkubwa kwa Waislamu.

Al-Fath ni jina la Sura ya 48 ya Qur'ani Tukufu. Ina Aya 29 na iko katika Juzzu ya 26. Al-Fath ni Sura Madani (imeteremshwa Madina) na ni sura ya 112 ya Quran iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Fath Mubin (ushindi wa dhahiri) lililotajwa mwanzoni mwa sura. Inahusu ushindi uliopatikana kutokana na Mkataba wa Hudaybiyyah katika mwaka wa sita baada ya Hijra. Mkataba ulioanzisha usitishaji vita wa miaka kumi ulitiwa saini kati ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na makafiri wa Makka.

Mkataba wa amani ulipelekea ushindi mkubwa kama vile kukombolewa Khaybar katika mwaka wa 7 Hijria na kukombolewa Makka katika mwaka wa 8 ambapo idadi kubwa ya makafiri walisilimu.

Maudhui kuu ya Surah Al-Fath ni kuhusu ujumbe wa ushindi wa Waislamu na Mwenyezi Mungu akimkumbusha Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na waumini neema yake kwao.

Vile vile ni pamoja na kumsifu Mtukufu Mtume (SAW) na waumini, kutoa ahadi nzuri juu ya dunia na akhera, kuwapa washirikina habari njema kuhusu kupata utulivu wa akili na kupata malipo ya imani yao na msamaha kwa wale wanaopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu , pamoja na kuwaonya makafiri na wanafiki.

Sura inaangazia zaidi hadhi ya juu ya Mtukufu Mtume (SAW) na inafafanua zaidi malengo ya wahyi na Risala (utume) wa Mtukufu Mtume (SAW.).

Sura inaanza kwa bishara njema ya ushindi wa dhahiri na inasisitiza kwamba ndoto aliyoota Mtukufu Mtume (SAW) kuhusu kuingia Makka (na kuwashinda makafiri) ingetimia.

Sura Al-Fath pia inazungumzia usumbufu unaosababishwa na wanafiki na kutaja baadhi ya visingizio visivyo na msingi wanavyotoa ili kuepuka kwenda kwenye medani ya vita na madai yao yasiyofaa.

Kisha Sura inatanguliza yale makundi ambayo haitakiwi kuwepo katika medani ya vita na kisha kutaja baadhi ya sifa za wafuasi wa Mtukufu Mtume (SAW).

Habari zinazohusiana
captcha