IQNA

Shakhsia katika Qur'ani/ 7

Balaamu mwana wa Beori; msomi aliyedanganywa

21:10 - October 27, 2022
Habari ID: 3475995
TEHRAN (IQNA) - Wasomi wanaoitafakari dunia na sababu za matukio ndani yake wanakuwa na nyenzo bora za kusonga mbele kwenye njia ya kiroho na ukamilifu kuliko watu wa kawaida.

Hata hivyo, hii pia inajenga uwajibikaji zaidi kwao na wasipokuwa waangalifu inaweza kusababisha mkanganyiko na uasi na kusababisha kupotoka. Balaamu, mwana wa Beori, ni mmoja wa wasomi kama hawa ambao Qur’ani Tukufu imewaashiria.

Balaamu alikuwa mwanachuoni wa Bani Israil na aliishi  eneo la Sham katika kijiji kimoja wakati wa Nabii Musa (AS). Alifuata dini ya Ibrahim (AS) na watu wakamjia kutabiri yajayo na kuwaombea dua.

Alikuwa mtu mwaminifu na hata Musa (AS) alimridhia kuwa menezaji wa kidini. Alikuwa na hali ya kiroho hivi kwamba maombi yake kwa Mwenyezi Mungu yalijibiwa mara moja.

Walakini, shakhsia yake na hadhi yake hiyo ilibadilika ghafula. Alipotoka na kufuata njia isiyo sahihi huku akipoteza hadhi yake yote ya kiroho baada ya kudanganywa na ahadi za Firauni. Alipotea kiasi kwamba aligeuka na kuwa mmoja wa wapinzani wakaidi wa Musa (AS).

Baadhi ya sababu nyingine pia zimetajwa kwa kupotoka kwake, ikiwa ni pamoja na Umormoni, kuwaongoza Bani Israel kwenye ufisadi, na kumuonea wivu Musa (AS).

Qur’ani Tukufu imeashiria kisa chake bila kumtaja:

“(Muhammad), Na wasomee khabari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua nazo. Na Shet'ani akamuandama, akawa miongoni walio potea.  Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.. (Aya ya 175-176 ya Surah Al-A'raf)

Ijapokuwa hakuna kutajwa kwa Balaamu katika aya hizi, baadhi ya ishara katika Aya pamoja na Hadithi zinaonyesha kwamba zinamrejelea Balaamu. Huenda moja ya sababu za kutomtaja ni kuonesha kuwa katika kila kipindi kuna wanachuoni mfano wake wajuzi na waongofu lakini ni wanyonge na waliopotea.

Balaamu na wanazuoni wengine wote wanaokubali tamaa za kidunia au wivu na kuweka uwezo wao wa kiroho na kiakili katika huduma ya madhalimu na wakandamizaji kwa hakika wanajidhulumu nafsi zao na hatima mbaya inawangoja.

captcha