IQNA

Waislamu India

India: Msikiti wa khistoria wabomolewa kwa ajili ya Upanuzi wa Barabara

20:31 - January 17, 2023
Habari ID: 3476418
TEHRAN (IQNA) – Mamlaka za India zimebomoa msikiti wa karne ya 16 huko Uttar Pradesh kama sehemu ya mradi wa kupanua barabara.

Shahi Masjid, msikiti wa karne ya 16 uliojengwa wakati wa utawala wa Sher Shah Suri ulibomolewa katika eneo la Handia la Prayagraj, Uttar Pradesh. Kulingana na idara ya kazi za umma ya Prayagraj, msikiti huo ulibomolewa ili kupanua barabara ya G T.

Cha kusikitishwa ni kwamba, imamu wa Msikiti huo, Md Babul Hussain alisema kwamba kesi hiyo iliorodheshwa katika mahakama ya chini hadi Januari 16. Lakini wakuu wa eneo wamechukua hatua ya kubomoa msikiti kabla ya kesi kusikilizwa.

Kesi hiyo ilifikishwa katika mahakama ya chini baada ya Mahakama Kuu ya Allahabad kutupilia mbali ombi la kusitisha ubomoaji huo Agosti, mwaka jana.

Klipu iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kubomolewa msikiti huo imepelekea wengi walaani  utawala wa wilaya na serikali ya Uttar Pradesh kwa kitendo hicho.

3482106

Kishikizo: india waislamu msikiti
captcha