IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /28

Sifa Maalum za Usomaji Qur'ani wa Ustadh Minshawi

20:21 - February 21, 2023
Habari ID: 3476596
TEHRAN (IQNA)- Alikuwa shakhsia mkubwa wa ulimwengu wa Kiislamu ambaye alianzisha mitindo mbalimbali ya usomaji wa Qur'ani Tukufu. Sauti yake nzuri na ustadi wake wa kutamka maneno kwa usahihi na kwa nguvu uliwasaidia wasikilizaji kuelewa maana ya mistari aliyokariri.

Minshawi alizaliwa Januari 20, 1920 katika mji wa Al Minshah katika Jimbo la Sohag nchini Misri, na alilelewa katika familia ya wasomaji wa Qur'ani.

Alijifunza Qur'ani nzima kwa moyo akiwa na umri wa miaka 8 na mwaka mmoja baadaye alianza kusoma Qur'ani.

Baada ya muda usio mrefu Minshawi akawa Qari mashuhuri katika mitindo ya Tahqiq na Tarteel.

Alisafiri katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Indonesia, Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Pakistan na Sudan, kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Minshawi aliaga dunia mnamo 1969 akiwa na umri wa miaka 49.

Wakati maafisa wa Idhaa ya Qur'ani ya Misri waliposikia sauti yake nzuri, walimwalika ajiunge na redio lakini Ustadh Minshawi alikataa kwa vile hakupendelea umaarufu.

Basi wakaenda nyumbani kwake kurekodi kisomo chake huko. Baada ya kutangazwa kwenye Redio ya Qur'ani, sifa zake zilienea kote Misri na katika nchi zingine za Kiislamu.

Usomaji wa Ustadh Minshawi ulikuwa na mwelekeo wa kiroho na adabu. Alizingatia sana maelewano kati ya maana na Lahn (toni) na alitilia mkazo juu ya kuzingatia kwa usahihi kanuni za Tajweed na Waqf na Ibtida (kutua na kuanza upya).

Alichagua kwa makini Lahn sahihi katika kuzisoma Aya kwa kuzingatia maana zake na ndio maana alitumia mitindo tofauti katika usomaji wake.

Kwa kuzingatia sauti yake maalum, Minshawi aliulikana kama Hanjarah al-Bakiya. Alikuwa akiisoma Qur'ani Tukufu kwa mtindo maalum ambao uliwaathiri sana wasikilizaji.

Kinachofuata ni kisomo chake cha Aya ya 38 ya Surah Baqarah:

captcha