IQNA

Umoja wa Kiislamu

Karzai: Kupambana na ugaidi kunaweza kuimarisha umoja wa Waislamu

18:35 - October 10, 2022
Habari ID: 3475910
TEHRAN (IQNA) - Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai anasema kupambana na itikadi kali na ugaidi ni suluhisho la kivitendo la kuimarisha umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia Kongamano la 36 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu siku ya Jumapili katika mkutano wa mtandaoni.

"Leo hii, ulimwengu wa Uislamu unapambana na matukio mawili mabaya ya itikadi kali na ugaidi, ambayo yanachukuliwa kuwa tishio kubwa kwa maslahi ya kidini na maslahi ya pamoja ya Waislamu. Matukio haya mawili mabaya yanaunganishwa na yanahusiana,” alisema.

Amebainisha kuwa misimamo mikali ni chanzo cha ugaidi na ugaidi ni sababu ya kueneza misimamo mikali na kubainisha kuwa, “Bila shaka, kuenea kwa itikadi kali kunafanyika kwa lengo la kupata maslahi ya kisiasa, ambayo husababisha hasara kubwa na uharibifu," Karzai aliongeza.

Kwa ajili ya suluhu la kivitendo la kuimarisha udugu na umoja katika jamii ya Kiislamu, alisisitiza: “Lazima tuzingatie kwa uzito na kwa kina nukta mbili za msingi: Kwanza, kujaribu kutatua mgongano wa kimaslahi katika uhusiano wa kimataifa, na pili, kupambana na misimamo mikali na misimamo mikali pamoja ugaidi.”

"Ninapendekeza kwamba kwa lengo la kuunganisha udugu, kuzuia ushawishi ajinabi katika uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na kufungua mlango wa maingiliano yenye manufaa na mataifa mengine, tunapaswa kufikiria juu ya kuandaa hati ya kimataifa ya misimamo ya wastani."

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imeaandaa toleo la 36 la Kongamano la Umoja wa Kiislamu ambapo ushiriki kupitia vikao vya itaneti au webinar ukiwa umeanza jana huku kongamano hilo likitazamiwa kufunguliwa rasmi 12 Oktoba na kuendelea hadi Ijumaa kwa kushirikisha wanazuoni wengi wa Kiislamu kutoka nchi 60.

Jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa kongamano la kimataifa la Umoja wa Kiislamu kila mwaka kwa muda wa miaka 35 sasa.

Kongamano hilo kwa kawaida hufanyika Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama siku za Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal.

Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu.

4090603

captcha