IQNA

Umoja wa Kiislamu

Kongamano London lajadili mizizi ya Chuki Dhidi ya Uislamu

14:24 - October 19, 2022
Habari ID: 3475952
TEHRAN (IQNA) – Mkutano mjini London umejadili chimbuko la Chuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia) , ukitoa wito kwa Waislamu kujenga umoja ili kukabiliana na hali hii.

Toleo la 24 la Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Umma lilifanyika tarehe 16 Oktoba katika Kituo cha Kiislamu cha Uingereza.

Wasomi na wanafikra kutoka Iran, Indonesia, Uingereza, Bahrain, na Pakistan walishiriki katika hafla ya mwaka huu.

Akihutubia mkutano huo, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Uingereza Hujjatul Islam Seyed Hashem Mousavi ameashiria ulazima wa kukabiliana na mgawanyiko katika ulimwengu wa Kiislamu.

"Kukuza mifarakano miongoni mwa Waislamu kunalenga kudhoofisha nguvu ya jamii ya Kiislamu," alisema.

Juhudi zozote dhidi ya umoja wa Umma wa Kiislamu ni huduma kwa maadui wa Uislamu na wasomi wa wanazuoni wa Kiislamu hawapaswi kukaa kimya, aliongezea Khatibu huyo.

Katika sehemu nyingine, akizungumzia chimbuko la chuki dhidi ya Uislamu, alibainisha kuwa maadui wanatumia mbinu tofauti kuendeleza chuki dhidi ya Uislamu ikiwa ni pamoja na kuutambulisha Uislamu kuwa ni dini yenye fujo na ghasia na inayounga mkono ugaidi na kuudhihirisha Uislamu kuwa ni dini isiyostaarabika na isiyo na mantiki.

Hujjatul Islam Mousavi amebaini kuwa suluhisho la kukabiliana na tishio hili, ni kuwafahamisha watu wa Ulaya kuhusu Uislamu wa kweli, kuandaa mazingira ya mazungumzo kati ya Waislamu na Wamagharibi wasio Waislamu, na kufanya jitihada za kuepuka misimamo mikali.

Mkutano huo ulifanyika sambamba na Wiki ya Umoja wa Kiislamu.

Siku ya 17 ya Rabi al-Awwal, iliyoangukia Oktoba 13 mwaka huu, inaaminika na Waislamu wa Shia kuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), huku Waislamu wa Sunni wakizingatia siku ya 12 ya mwezi (Jumapili, Oktoba 9) kama siku ya kuzaliwa nabii huyo wa mwisho.

Muda kati ya tarehe hizo mbili huadhimishwa kila mwaka kama Wiki ya Umoja wa Kiislamu.

Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini (RA) ndiye aliyekuja na ubunifu huo wa kutangaza Wiki ya Umoja wa Kiislamu miaka ya 1980.

4092623

captcha