IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Uswidi kumfukuza mchochezi aliyechoma moto nakala za Qur'ani Tukufu

20:50 - October 27, 2023
Habari ID: 3477796
STOCKHOLM (IQNA) - Mamlaka za Uswidi zimeamua kumfukuza raia wa Iraq ambaye alivunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika maandamano ya hadhara katika miezi ya hivi karibuni.

Salwan Momika, ambaye alikuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini Uswidi, atafukuzwa nchini Aprili 16, kulingana na Jesper Tengroth, msemaji wa Ofisi ya Uhamiaji.

Aliiambia TV4 kuwa Momika alitoa taarifa za uongo katika maombi yake ya vibali hivyo. Pia alisema kuwa Momika atapigwa marufuku kuingia Uswidi kwa miaka mitano.

Momika anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kupeleka kesi katika mahakama ya uhamiaji.

Tengroth, hata hivyo, aliongeza kuwa kuna "kizuizi cha kutekeleza amri hiyo," akisema kwamba Momika anaweza kuadhibiwa katika nchi yake ya asili, Iraq.

Momika alizua hasira alipochoma nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya Ubalozi wa Uturuki nchini Uswidi mnamo Juni 21. Alirudia kitendo hicho kiovu wiki moja baadaye nje ya msikiti mmoja huko Stockholm wakati wa Eid al-Adha, sherehe kubwa ya kidini ya Kiislamu.

Tangu wakati huo, amerudia vitendo hivyo viov huo katika matukio mengi katika miji mbalimbali ya Uswidi, ya hivi punde zaidi ikiwa ni Oktoba 21 huko Stockholm.

Uswidi, pamoja na Denmark na Uholanzi, zimekabiliwa na shutuma nyingi kwa kuruhusu kuchafuliwa hadharani kwa Quran chini ya ulinzi wa polisi.

3485755

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu uswidi
captcha