IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Taarifa ya serikali ya Uswidi kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

16:46 - July 03, 2023
Habari ID: 3477229
STOCKHOLM (IQNA) - Serikali ya Uswidi (Sweden) Jumapili ilitoa taarifa baada ya nakala ya Qur'ani Tukufu kuchomwa moto nje ya msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo, Stockholm.

"Serikali ya Uswidi inaelewa kikamilifu kwamba vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vinavyofanywa na watu binafsi kwenye maandamano nchini Uswidi vinaweza kuwakera Waislamu," wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa yake.

"Tunalaani vikali vitendo hivi, ambavyo havionyeshi kwa vyovyote maoni ya serikali ya Uswidi," iliongeza.

“Kuchomwa moto kwa Qur’an, au maandishi yoyote matakatifu, ni kitendo cha kuudhi na kisicho na heshima na ni uchochezi wa wazi. Maneno ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na ukosefu wa uvumilivu unaohusiana hayana nafasi nchini Uswidi au Ulaya," wizara ya mambo ya nje ya Uswidi ilisema.

Kauli hiyo imekuja baada ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kusema Jumapili kwamba hatua za pamoja zinahitajika ili kuzuia vitendo vya kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu na kwamba sheria za kimataifa zitumike kukomesha chuki za kidini baada ya kitabu hicho kitakatifu kuchomwa moto katika maandamano nchini Sweden.

Siku ya Jumatano, mtu mmoja aliirarua na kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya msikiti mkuu wa Stockholm siku ya Jumatano, siku ya kwanza ya sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha.

4152001

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha