IQNA

Uswidi: Waislamu waandamana kulaani uchomaji wa Qur'ani Tukufu

21:34 - July 10, 2023
Habari ID: 3477262
STOCKHOLM (IQNA) - Mamia ya Waislamu huko Uswidi wameandamana katika mji mkuu, Stockholm kulaani kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Ulaya.

Mji mkuu wa Sweden ulishuhudia maandamano makubwa siku ya Jumapili, ambapo Waislamu waliandamana kupinga matukio ya hivi majuzi ya uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu nchini humo.

Maandamano hayo yaliandaliwa na makundi ya Waislamu katika Medani ya Medborgarepaltsen mjini Stockholm, ambapo waandamanaji wapatao 500 walitoa wito wa kupigwa marufuku kisheria vitendo hivyo vya kutoheshimu kitabu kitakatifu cha Uislamu.

Waandaaji hao wamesema katika taarifa yao kuwa kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni kitendo cha chuki na chuki dhidi ya Uislamu ambacho kinaumiza hisia za Waislamu na kwamba vitabu vitakatifu vinapaswa kulindwa ili visivunjiwe heshima.

Mikail Yuksel, kiongozi wa chama cha Nyans (Nnuance), aliiambia Shirika la Habari la Anadolu kwamba uchomaji wa Qur'ani Tukufu haukubaliki kisheria.

Alisema kuwa vitendo hivyo vinapaswa kuchukuliwa kuwa uhalifu wa chuki na kwamba havina nafasi katika jamii za kidemokrasia. Aliomba marekebisho ya kisheria kuhusu suala hilo.

Mwezi uliopita, mwanamume mmoja alichoma nakala ya  Qur'ani Tukufu chini ya ulinzi wa polisi mbele ya Msikiti wa Stockholm.

Alichagua kufanya kitendo hicho kiovu katika siku kuu ya ya Eid al-Adha, mojawapo ya sherehe muhimu za Kiislamu zinazoadhimishwa na Waislamu duniani kote.

Kitendo chake kilizua hasira na kulaaniwa na nchi nyingi za Kiislamu, zikiwemo Iran, Uturuki, Saudi Arabia, Iraq, Pakistan, na Morocco.

Mnamo Januari, uchomaji mwingine wa Qur'ani Tukufu ulifanywa na mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia nje ya Ubalozi wa Uturuki nchini Uswidi.

3484278

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha