IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Marais wa Iran na Algeria wajadili njia za kukabilina na vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu

15:30 - July 01, 2023
Habari ID: 3477223
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mataifa ya Waislamu yana wajibu na jukumu la kulaani na kupinga vitendo vya nchi za Magharibi vya kuvunja heshima matukufu ya Kiislamu, hususan Qurani Tukufu.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu ya mwenzake wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune ambapo mbali na kumpa mkono wa kheri kwa mnasaba wa sikukuu ya Iddul Adh'ha, amesisitiza kuwa Waislamu katika maeneo yote ya dunia wameeleza kuchukizwa kwao na uovu huo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sanjari na kulaani kitendo hicho cha kudhalilishwa Qur'ani Tukufu nchini Sweden amesema kuwa serikali yake ina hamu ya kuimarisha uhusiano na mataifa ya Kiislamu na nchi rafiki duniani.

Kadhalika Sayyid Ebrahim Raisi amesema Jamhuri ya Kiislamu inatumai kuwa uhusiano na ushirikiano wa pande mbili baina ya nchi hii na Algeria utaimarishwa zaidi, hasa katika nyuga za uchumi na biashara.

Kwa upande wake, Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune amesisitizia haja ya kulindwa nembo na matukufu ya Kiislamu kote duniani. Aidha amesema nchi yake iko tayari kuimarisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu katika nyuga tofauti.

Mataifa mengi ya Waislamu kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Iraq, Saudi Arabia, Kuwait, Pakistan, Jordan na Uturuki yametoa taarifa za kulaani kitendo hicho cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi au (Sweden).

4151451

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu uswidi
captcha