IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti Uswidi wapokea bahasha ya kutisha, polisi waanzisha uchunguzi

8:14 - August 19, 2023
Habari ID: 3477460
STOCKHOLM (IQNA) - Polisi huko Gothenburg, Uswidi, wanachunguza kesi ya uhalifu wa chuki baada ya msikiti mmoja kupokea bahasha ya kutisha iliyokuwa na unga mweupe siku ya Ijumaa.

Jumuiya ya Utamaduni wa Kiislamu ya Gothenburg, ambayo inaendesha msikiti huko Hisingen, iliripoti tukio hilo kwa polisi baada ya sala ya Ijumaa.

Rais wa chama hicho, Faraj Semmo, alisema alifungua bahasha na kupata unga huo mikononi mwake. Aliiambia Televisheni ya SVT kwamba hakutaka kuwashtua waumini na akasubiri hadi walipoondoka ili kuwaita polisi.

Polisi walisema wamekamata bahasha na unga huo kwa ajili ya uchunguzi.

Tukio hilo limetokea wakati nchi hiyo ya ukanda wa Nordic ikishuhudia kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu katika wiki chache zilizopita huku watu wenye misimamo mikali wakiendesha mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu licha ya kulaaniwa kimataifa.

3484825

Habari zinazohusiana
captcha