IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Katibu Mkuu wa OIC anaonya kuhusu kiwango cha 'Kutisha' cha chuki dhidi ya Uislamu

18:16 - February 01, 2023
Habari ID: 3476500
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ametahadharisha juu ya kiwango cha kutisha cha chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia )kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Ulaya hivi karibuni.

Alisema hayo wakati OIC ilipoitisha kikao cha wazi cha kamati yake tendaji katika makao yake makuu mjini Jeddah siku ya Jumanne.

Mkutano huo ulifanyika ili kuelezea msimamo wa pamoja wa shirika hilo la nchi za Kiislamu kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Uswidi, Uholanzi na Denmark na pia kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa na OIC dhidi ya wahusika wa chuki dhidi ya Uislamu.

Katibu Mkuu wa OIC Hissein Brahim Taha alisema kuwa vitendo hivi sio tu vya kutowajibika bali ni vitendo vya uhalifu vinavyolenga Waislamu. "Serikali zinazohusika lazima zichukue hatua kali za kuadhibu, hasa ikizingatiwa mara kwa mara vitendo hivyo vya uchochezi vinavyofanywa na watu hao hao," alisema.

"Vitendo vya kuchukiza…ni ushahidi zaidi wa viwango vya kutisha vilivyofikiwa na hali ya chuki dhidi ya Uislamu, uhalifu wa chuki, kutovumilia na chuki ya wageni.

"Hii inatufanya tuamini kwamba lazima tuchukue hatua za haraka ili kuzuia kujirudia kwa matukio kama haya ya uchochezi katika siku zijazo."

Taha alisema kuwa ni lazima ujumbe mzito upelekwe kwa serikali zote, taasisi na watu binafsi kufafanua kuwa vitendo hivyo ambavyo havina uhalali chini ya uhuru wa kujieleza. Alisisitiza kwamba sheria nyingi za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, zinaeleza wazi kwamba uhuru wa kujieleza si haki isiyo na kikomo, kwani unahusisha wajibu na wajibu maalum.

3482308

Habari zinazohusiana
captcha