IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Polisi wa Uswidi wazuia uchomaji nakala ya Qur’ani Tukufu wakihofia usalama

20:16 - February 17, 2023
Habari ID: 3476575
TEHRAN (IQNA) - Polisi katika mji mkuu wa Uswidi (Sweden) wa Stockholm wamekataa ombi la maandamano ya kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya ubalozi wa Iraq.

Kuvunjiwa heshima kwa Qur’ani Tukufu kulipangwa kuandaliwa siku ya Alhamisi. "Uamuzi huo unahalalishwa kwa misingi kwamba maandamano hayo yanaweza kusababisha tishio la kigaidi nchini Uswidi," SVT Nyheter iliripoti.

"Kwa ujumla, Huduma ya Usalama inaamini kuwa uchomaji wa nakala ya  Qur'ani Tukufu yenyewe umeongezeka, na huenda ikaongeza tishio la mashambulizi dhidi ya Uswidi na maslahi ya Uswidi katika muda mfupi," uamuzi wa polisi, ambao ulichukuliwa kwa kushauriana na Huduma ya Usalama wa Uswidi inayojulikana kama Säpo, inasema.

Ripoti hiyo inakuja huku weledi wa mambo wakiamini kuwa vitendo vya mara kwa mara vya kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu vinaweza kuvuruga azma ya Uswidi ya kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO.

Kiongozi wa chama cha siasa cha  chenye misimamo mikali ya kufurutu ada cha  Stram Kurs kutoka Denmark, Rasmus Paludan, alichoma nakala ya Qur’ani Tukufu huko Stockholm, Uswidi, Januari 21. Kitendo hicho kichafu na cha jinai kilijiri wakati Paludan alipoandamana mbele ya Ubalozi wa Uturuki kuhusu uanachama wa NATO wa nchi hiyo ya Nordic. .

Uswidi na nchi jirani ya Finland zinataka kujiunga na muungano wa kijeshi huku kukiwa na vita nchini Ukraine, hatua inayomaanisha zinajiondoa katika sera ya kihistoria ya kutofungamana na upande wowote.

Hata hivyo, kujiunga kwao kungehitaji idhini kutoka kwa wanachama wote wa NATO, na Uturuki imeonyesha kuwa itazuia jitihada za Uswidi - kwa sehemu kutokana na kitendo hicho Paludan.

Hata kabla ya hapo, Ankara ilikuwa inashinikiza nchi hizo mbili kukabiliana na makundi yenye silaha ya Kikurdi na wanaharakati na makundi mengine ya kigaidi ambao wanachama wao wanaishi katika nchi hizo mbili

Wakati huo huo, vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu Uswidi na nchi zingine za Ulaya vimelaaniwa vikali katika nchi za Kiislamu duniani kote ambazo pia zimeitaka serikali ya Uswidi kuzuia matukio kama hayo la sivyo bidhaa za nchi hiyo zitasusiwa na Waislamu duniani kote.

 4122676

captcha