IQNA

Kongamano

Washiriki wa mkutano wa kimataifa kuhusu vyombo vya habari, Umoja wa Waislamu walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

17:30 - January 30, 2023
Habari ID: 3476487
TEHRAN (IQNA) - Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa vyombo vya habari na umoja wa Umma wa Kiislamu umefanyika hapa katika mji mkuu wa Iran siku ya Jumatatu.

Imeandaliwa na Kituo cha Wanaharakati wa Vyombo vya Habari vya Ulimwengu wa Kiislamu kwa usaidizi wa Jukwaa la Kimataifa la Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.

Wanaharakati wakuu wa vyombo vya habari na wasomi wa kidini kutoka zaidi ya nchi 20 wamehudhuria hafla hiyo wakijadili masuala yanayohusiana na umoja wa Umma wa Kiislamu, ujuzi wa vyombo vya habari, na uwezo wa vyombo vya habari vya kimataifa.

Ni moja katika mfululizo wa mikusanyiko ya kimataifa inayoitwa Kongamano la Kimataifa la Mnara.

Washiriki wa hafla ya leo katika taarifa yao wamelaani vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima  Qur'ani Tukufu na matukufu ya Kiislamu katika nchi za Ulaya.

Walitaja hatua hizo za kufuru kuwa matendo ya aibu ambayo hakuna sheria au mantiki inayounga mkono.

Hatua hizo zinaumiza hisia za mabilioni ya Waislamu na watu mashuhuri duniani na kuibua chuki na mifarakano, walisema.

Taarifa hiyo pia ilizikashifu serikali za Magharibi kwa kupandikiza mbegu za chuki na uhasama na kuchochea moto wa ghasia duniani.

Ilisisitiza kwamba Waislamu, kwa msingi wa imani yao ya kidini, kamwe hawajiruhusu kutukana utakatifu wa imani nyingine na kwamba wafuasi wa Uislamu wanaviheshimu sana vitabu na manabii wote wa Mungu.

Participants in Int’l Conference on Media, Muslim Unity Denounce Desecration of Islamic Sanctities in West

Iran to hold 1st Minaret international conference

4118238

captcha