IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Aliyevunjia heshima Qur'ani Tukufu Uswidi kutimuliwa nchini humo

18:43 - February 09, 2024
Habari ID: 3478324
IQNA-Mahakama ya Uhajiri ya Uswidi (Sweden) imetangaza kwamba, mtafuta hifadhi wa Iraq, ambaye amefanya vitendo kadhaa vya kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, atafukuzwa nchini humo.

Ripoti zinasema serikali ya Uswidi hatimaye imeamua kumfukuza Salwan Momika, mkimbizi kutoka Iraq, kwa sababu ya kukabiliwa na msimamo mkali na malalamiko ya kidiplomasia na ya Waislamu karibu bilioni mbili kote duniani kutokana na kuendelea kumkingia kifua mhalifu huyo aliyevunjia hehima Qur'ani Tukufu, na ilikuwa ikikaribia kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa kidiplomasia na kiuchumi.

Hii ni pamoja na ukweli kwamba, Wasweden wengi hawakubaliani na kuchomwa moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani, na zaidi ya nusu ya waliohojiwa katika kura ya maoni ya hivi majuzi ya Mtandao wa Umma wa Uswidi walisema wanaunga mkono marufuku ya kuchomwa vitabu vitakatifu kama Qur'ani.

Oktoba mwaka jana (2023) Idara ya uhamiaji ya Uswidi ilikataa kuongeza muda wa kibali cha kuishi nchini humo Salwan Momika, lakini amri yake ya kuondolewa ilicheleweshwa kwa sababu za kiusalama.

Uamuzi huu ulitolewa baada ya kubainika kuwa Momika alikuwa ametoa taarifa za uongo katika takwa lake la kuomba hifadhi.

Mvunjiaji heshima huyo wa Qur’ani Tukufu alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, lakini rufaa yake ilikataliwa na majaji wa Uswidi. Kwa mujibu wa uamuzi huo, majaji waliamua kumpa Momika kibali cha muda cha kukaa ambacho muda wake unatarajiwa kumalizika Aprili 16 mwaka huu.

Salwan Momika, ambaye alichoma moto kitabu kitakatifu cha Qur’ani katika sikukuu ya Eidul Adh’ha mbele ya msikiti mkuu wa Stockholm kwa tamaa ya  kupata uraia wa Uswidi, hivi karibuni alidai kwamba polisi wa Uswidi hawakumuunga mkono tena na kumfanya kuwa mawindo rahisi kwa Waislamu.  Hata hivyo mhalifu huyo alirudia kitendo cha kuchoma moto nakala ya Qur’ani tukufu mara kadhaa na kila mara alipatiwa himaya na uungaji mkono kamili wa polisi.

Inaonekana kuwa, licha ya uungaji mkono wa mara kwa mara wa serikali na polisi ya Uswidi kwa Salwan Momika katika kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, lakini mashinikizo ya nchi za Kiislamu na hata Umoja wa Mataifa kwa upande mmoja, na vikwazo dhidi ya Uswidi na nchi za Kiislamu kwa upande mwingine dhidi ya nchi hiyo ya Skandinavia ni mambo ambayo yamewafanya maafisa wa nchi hiyo kuamua kuachana haraka na shari ya mhalifu huyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi za Ulaya hususan za eneo la Skandinavia zimekuwa uwanja wa ukiukaji na kuvunjiwa heshima matakatifu ya Waislamu. Tangu mwanzoni mwa majira ya kiangazi ya 2023, kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kwa namna ya uchomaji Qur'ani kumetokea mara nyingi katika nchi mbili za kaskazini mwa Ulaya, yaani Uswidi na Denmark, na baadhi ya watu wenye chuki dhidi ya Uislamu kama vile Salwan Momika na wafuasi wa vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo ya kufurutu ada.

Chini ya himaya na usaidizi wa polisi ya Uswidi na Denmark, watu hawa walichoma moto Quran Tukufu na maandamano ya Waislamu ya kulaani vitendo hivyo pia yalizimwa na kukandamizwa. Baada ya Salwan Momika kuitusi Quran Tukufu, ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad ulishambuliwa na waandamanaji wenye hasira na kuchomwa moto.

Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kumekabiliwa na wimbi la malalamiko makubwa hususan katika ulimwengu wa Kiislamu na kupelekea maandamano makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na nchi nyinginezo. Kuhusiana na hilo  hivi karibuni Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilizitaka nchi wanachama kuchukua hatua zinazofaa za kisiasa na kiuchumi dhidi ya Uswidi na nchi nyinginezo ambazo zinaruhusu kuchomwa vitabu vitakatifu vya Kiislamu.

3487128

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha