IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mufti wa Oman atoa wito wa kususiwa bidhaa za Uswidi kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

19:17 - July 02, 2023
Habari ID: 3477228
MUSCAT (IQNA)- Mufti wa Oman ametoa wito wa kususiwa bidhaa za Sweden kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Uswidi (Sweden).

Jumatano mchana tarehe 28 mwezi Juni raia wa Uswidi aliyejukana kwa jina la Salwan Momika (37) alichoma moto na kuchana nakala ya Qur'ani Tukufu huko Stockholm mji mkuu wa nchi hiyo katika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Idul-Adh'ha. Momika alitenda jinai hiyo baada ya polisi wa Uswidi kumpa kibali cha kufanya maandamano dhidi ya Uislamu. 

Sheikh Ahmad bin Hamad al Khalili, Mufti wa Oman, leo amepinga vikali kitendo hicho cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu na kusema: Waislamu popote walipo Mashariki na Magharibi mwa dunia, wanapasa kukabiliana na jinai hiyo. Amesema, 'jambo dogo zaidi wanalopasa kufanya dhidi ya uhalifu huu mkubwa ni kususia kabisa  bidhaa za Uswidi.'  

Mufti wa Oman amewatolea wito Waislamu duniani kote kususia bidhaa za Uswidi. na kuzitaka taasiisi na jumuiya zote za Kiislamu zikiwemo serikali za nchi kufutilia mbali ushirikiano wa kibiashara na kifedha na nchi hiyo ya eneo la Skandinavia barani Ulaya.

Baadhi ya nchi za Kiislamu zikiwemo Pakistan,  Uturuki na Yemen pia sambamba na kuendelea kulaani kitendo hicho cha kishetani cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Sweden, zimetaka kususiwa bidhaa kutoka Sweden. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza haitamtuma balozi wake mpy Uswidi kufuatia kuvuniwa heshima Qur'ani Tukufu nchini humo.

3484171

captcha